Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza amekutana na wenyeviti wa mitaa yote ya Jiji la Mwanza
Katika kikao chake hicho na wenyeviti, amewaomba kuisadia Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupata takwimu sahihi za vizimba na Nyumba za kulala wageni zilizoko kwenye mitaa yao.
Aidha Mheshimiwa Bwire amewataka watendaji wote wa mitaa kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa katika kutekeleza maagizo mbalimbali wanayopokea.
"Kama Halmashauri tunawahamasisha muendelee kuibua maendeleo kwenye kata kama ujenzi wa madarasa, zahanati na ofisi za mitaa na sisi tutamalizia" amesema Mheshimiwa Bwire
Wakati huo huo Naibu meya wa Jiji la Mwanza Mheshimiwa Kotecha amewaomba wenyeviti kujitokeza kutia shime timu ya "Alliance Sports Club" katika jitihada zake za kucheza ligi kuu.
Kikao hiki kinaashiria mwanzo mpya wa utendaji kazi kati ya Halmashauri ya Jiji na wenyeviti wa mitaa
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.