Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba leo ameambatana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ya Nyamagana kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika soko la muda la Mbugani.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt.Phillis Nyimbi amewataka wafanyabiashara ndogondogo machinga wanaovamia na kujenga Juu ya mitaro ya maji kuacha mara moja kwani uweza kusababisha mafuriko wakati wa masika.
Aidha Dkt.Nyimbi amewahasa wafanyabiashara hao kuwa na subira na kusubiria kwanza soko kujengwa.
Akiongea na wafanyabiashara hao wadogo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba amesema wafanyabiashara hao wadogo wanatakiwa kuhakikisha sana vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo .
Lakini pia Mkurugenzi amewahasa wafanyabiashara hao kutokuzinga biashara za wenye maduka
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.