KAMATI YA FEDHA YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MIRADI YA UMILIKISHAJI WA VIWANJA - LUCHELELE
KAMATI ya fedha Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo imefanya ziara katika maeneo ya Upangaji, Upimaji na umilikishaji wa viwanja eneo la Luchelele pamoja na Maendeleo ya ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Msingi Mabatini.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe, Lodrick Ngoye amewataka Idara ya Mipango miji, kitengo cha Ardhi Jiji kuhakikisha wanakamilisha uthaminishaji, upangaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi wa Luchelele wanaotakiwa kupisha mradi wa viwanja hivyo.
“Mradi huu ni wa kimkakati na unatakiwa ukamilike kwa wakati ili uuzaji wa viwanja uanze mara moja na Jiji lianze kupata mapato yake ili fedha hizo zisaidie baadae katika upimaji wa maeneo mengine ya uwekezaji" Mhe. Ngoye
Awali akitoa maelezo juu ya mradi huo, Afisa Ardhi Mteule Bi. Halima Nassoro amesema Jiji lilipokea kiasi cha zaidi ya Tsh.Millioni 800 kutoka Wizara ya Ardhi kwa ajili ya Upangaji, upimaji na umilikishaji wa viwanja 541 eneo la Luchelele.
Ameongeza kuwa, mara baada ya kupokea kiasi hicho wameweza kupima jumla ya viwanja 715 huku zaidi ya wakazi 100 wakitakiwa kulipwa fidia ya zaidi ya Tsh. Milioni 600 ili kupisha maeneo ya mradi.
“Kwa sasa tumeipitia michoro ya mipango miji na wataalam wako site kwa ajili ya kupanda bikoni ili kuzipa ramani ili kuweza kutangaza na kuanza kuuza viwanja vilivyo katika mandhari nzuri ya uwekezaji wa Hoteli, shule, Majengo mall na maeneo safi ya kuishi,”amesema Bi. Nassoro.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.