Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe.Mussa Sima amefanya ziara ya kikazi Jijini Mwanza kwa kulitembelea Dampo la kisasa lilopo Kata ya Buhongwa.
Akikagua ujenzi wa Dampo la kisasa Mhe.Sima amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa kusimamia ujenzi wa Dampo la kisasa la Buhongwa.
Mhe Sima amesema kwa Dampo hilo kujengwa kutasaidia kupunguza mlipuko wa magonjwa na itasaidia katika utunzaji wa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba amesema awali Dampo lilikuwa na uwezo wa kukusanya tani 30 mpaka tani 35 kwa siku lakini kukamilika kwa ujenzi wa Dampo la kisasa ukusanyaji wa taka pia utaongezeka
Amesema ujenzi wa Dampo la kisasa unajumuisha ujenzi wa mizani ya kupimia taka, uzio, mefereji ya kuzuia maji ya mvua , sehemu ya kuoshea magari
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.