Baraza la Halmashauri la Jiji la Mwanza limekaa kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji shughuli za maendeleo katika Kata zote za Halmashauri ya jiji la Mwanza .
Akizungumza wakati wa kufunga Baraza hilo Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ameipongeza Idara ya ardhi kwa kufanya vizuri katika zoezi la urasimishaji makazi ambapo viwanja 19000 vimepimwa
Aidha Mstahiki meya amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la mwanza kutoa zaidi ya Milioni Mia moja kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Mwisho Mstahiki meya amesema kuwa Halmashauri yake ina upungufu mkubwa wa madawati pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na mkurugenzi kutengeneza madawati, hivyo amemuomba Mkuu wa wilaya kuwahamasisha wadau mbali mbali wa maendeleo kuchangia
Akitoa Salamu zake Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, amewataka watumishi pamoja na wananchi kujitokeza kumpokea na kumsikiliza waziri Mkuu ambaye atakuwepo Nyamagana tarehe 20/02/2018 eneo la Bulale kata ya Buhongwa.
Aidha Mkuu wa wilaya amewataka waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa Mitaa kuwahamasisha wananchi kuchangia masuala ya maendeleo
Akitoa salamu zake Naibu Meya wa Jiji la Mwanza , Mheshimiwa Bhiku Kotecha aameipongeza timu ya alliance sports club kupanda ligi kuu ya Tanzania bara 2018/2019 . mheshimiwa kotecha amehaidi kama Baraza la Madiwani la Halmashauri litatoa Ushirikiano wa kutosha kwa timu ya alliance
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.