Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Umma imetoa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara, Watendaji Kata Mitaa, na Wenyeviti wa Mitaa.
Mafunzo haya yalianza kutolewa tarehe 29/05/2017 katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza .Lengo la Mafunzo ni kuwafanya Viongozi na Watumishi wa Umma kuishi kwa kufuata miiko ya Uongozi na Maadili ya Utumishi wa Umma.
Katika Mafunzo hayo Viongozi na Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya Maamuzi sahihi kwa kuzingatia Sheria Kanuni na taratibu ili kuepuka uonevu na kuingizwa kwenye migogoro isiyokuwa na tija.
Aidha Vingozi wa Umma wameaswa Kufuata Utaratibu wa Kisheria katika kumuwajibisha Mtumishi wa Umma anapokuwa amekosea “Si vyema kumdhalilisha mtumishi wa Umma hadharani anapokuwa amekosea, jambo la msingi ni kufuata taratibu na sheria “ alisema Muwezeshaji
Viongozi na Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili wawapo ndani ya Kazi na Nje ya kazi , Maana Utumishi ama cheo hakifutiki mtu awapo Nje, na afahamu anapokiuka maadili anaharibu taswira yake mwenyewe na Taswira ya taasisi husika.
Aidha Viongozi wametakiwa kutovujisha taarifa mbalimbali za vikao kabla , hazijaamuliwa na mamlaka husika kutolewa kwa wananchi, “ Halmashauri ina watu mahususi wa Kutoa taarifa kwa wananchi si kila Mtu ni Msemaji wa Taasisi, Kuna Maafisa habari ambao wameajiriwa mahususi kwa kazi hiyo” alisema Muwezeshaji
Wakizungumza na Watumishi na Viongozi wa Umma, Maafisa wa Takukuru kitengo cha Elimu kwa Umma wamesema athari za rushwa kwenye jamii yetu ni kubwa na hupelekea wananchi kuilaumu serikali kwa kutokupata huduma za Jamii kwa sababu ya baadhi ya watumishi na viongozi wa umma wapenda Rushwa wanaosababisha miradi mbambali ya maendeleo kukamilika kwa kiwango cha chini
“Kwa Sababu ya Rushwa Haki za watu hupotea, Madawa hayapo, Elimu inakufa, Watu inabidi tubadilike, Rais wetu hataki uzembe na anachukia Rushwa”
Semina hii imetolewa na serikali kuhakikisha Viongozi pamoja na watumishi wa Umma wanawahudumia watanzania kwa namna inayofaa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.