Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha jana tarehe 4.05.2017,alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali itakayozinduliwa /kufunguliwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 katika wilaya ya Nyamagana
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya aliambata na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba,ambapo katika ziara hiyo miradi mbalimbali ilikaguliwa na kutolewa maelekezo kwa ajili ya kuiboresha zaidi
katika kata ya Mhandu Mkuu wa wilaya alipata fursa ya kutembelea kiwanda kidogo cha kutengenezea magodoro kinachomilikiwa na mjasiriamali Yahaya Tosi ambae alionesha namna yakutengeneza magodoro na changamoto mbalimbali anazokumbana nazo
Mkurugenzi wa jiji la mwanza alivutiwa na juhudi zinazofanywa na Ndg Haji Yahaya,na alimtaka kufika katika ofisi zaJiji la Mwanza kwa ajili ya kuonana na wataalamu ili wamsaidie namna ya kupata mkopo wakuboresha kiwanda chake.
Aidha Mkuu wa wilaya alitembelea mradi wa dampo uliopo Buhongwa ambapo alijionea nakupata maelezo ya kina ya mradi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,pia mradi wa ujenzi wa Barabara ya mawe katika kata ya Pamba.
Pia alitembelea eneo ambalo Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatarajia kujenga wodi ya wanawake na watoto katika hospitali ya Nyamagana iliopo kata ya Butimba.
Katika ziara hiyo piaalitembelea mradi wamaji katika eneo la Fumagila ,ambapo kwa sasa mkandarasi yuko katika hatua za mwisho za kukabidhi mradi huo kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,pia Mkuu wa wilaya alishuhudiawananchi wakichota maji.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.