Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndugu Kiomoni Kibamba Kiburwa amechaguliwa kwa sauti moja na wakurugenzi wa Halmashauri za miji, wilaya, Manispaa na Majiji kuwa mwenyekiti wao katika uchaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.
Uchaguzi huo umefanyika mara baada ya kumalizika kikao kazi kilichoongozwa na katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI )Mhandisi Musa Iyombe kilichohudhuriwa na wakurugenzi wote 185.
Baada ya kikao hicho wakurugenzi wote waliamua kuwa na wawakilishi ambao watakuwa wanawawakilisha na kufikisha changamoto zao katika ngazi za juu .Hivyo wakaamua kuwa na viongozi katika nafasi Nne ambazo ni Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti, Katibu, na Muweka Hazina.
Katika nafasi ya Mwenyekiti amechaguliwa Ndugu Kiomoni Kibamba Kiburwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Nafasi ya Makamu Menyekiti amechaguliwa Bi Rachel Chuwa – Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Nafasi ya Ukatibu amechaguliwa Ndugu Claire Shija- Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Nafasi ya Muweka Hazina kachaguliwa Ndg John Lipesi Kayombo –Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi hao waliochaguliwa wameeleza namna bora ya kuhimiza uwajibikaji kwa wakurugenzi wote sambamba na kuwawakilisha vyema katika kufikisha changamoto zao katika ngazi za juu.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.