Halmashauri ya Jiji la Mwanza yafunga mikataba na kandarasi walioshinda zabuni mbalimbali zilizotangazwa na Halmashauri ya Jiji la mwanza Mwezi Machi, Utiaji saini huo umefanyika katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ambao ulihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji na Timu ya Menejimenti ya halmashauri. Zabuni zilizotolewa ni Uwekaji wa taa za Barabarani Barabara ya Rwagasore, Machemba ,Nasa drive,Regional drive,Rufiji,Mission, Barabara ya SAUT na Uhuru.
Tofauti na hiyo zabuni pia imetolewa zabuni ya Ujenzi wa sehemu korofi kama Posta – A, Mabatini, Unguja A, Isamilo- Mlimani, Isengeke, RIDEP , Daraja la Mesa sekondari, Butimba – Tafiri, Mkuyuni – Relini.
Wakati huo pia zabuni ya ujenzi wa vipindi maalumu imetolewa ambayo itahusisha Isamilo international – Mwananchi.
Zabuni ya Ujenzi wa madaraja pia imetolewa ambayo itahusisha Maina-Relini, Kona ya Igoma Kishiri, Mwananchi, Ipuli na Kokoto Mabatini, pamoja na ujenzi wa Barabara ya mawe “Catholic Church”
Akizungumza wakati wa utianaji saini kwenye mikataba Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg James Bwire amesema “Tutafuatilia na kuangalia utendaji kazi wenu, Hatutasita kusitisha zabuni zenu endapo kazi zenu hazitakidhi viwango”
Pamoja na hayo aliwaomba makandarasi kutosita kufika Ofisini kwake endapo watakutana na vikwazo vinavyowashinda kutekeleza majukumu yao.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba kiburwa aliwapongeza wakandarasi hao kushinda zabuni, na kuwataka kupiga kazi kwa vigezo walivyowekeana kwenye mikataba na kusema “ Tuna Maabara ya Kisasa hapa Jiji hivyo tutapima sampuli ya vifaa vyenu vya ujenzi, hatutasita kuwabomolea wote ambao hawakujenga kwa vigezo tulivyokubaliana”
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.