Katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo amewataka wakandarasi wa maji nchini kufanya kazi kwa weledi ili kuwa saidia wananchi kuondokana na adha ya kukosa maji
Prof kitila aliyasema hayo alipokuwa akifunga kikao kazi cha wahandisi wa maji wa halmashauri mbalimbali yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,Kikao hicho kilihudhiuriwa na Wahandisi wa Maji kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini.
Akiongea katika kikao kazi hicho Prof amesisitiza umuhimu wa kutumia uzoefu walioupata kuisaidia serikali kutatua changamoto ya ukosefu wa Maji kwa wananchi wake,pia kutumia mafunzo hayo kuwasimamia ipasavyo wakandarasi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika ngazi ya Halmashauri inakuwa na tija.
Kikao kazi hicho kilianza tarehe 11/07/2017 na kufikia tamati leo tarehe 13/07 2017
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.