Kamati ya wataalamu washauri wa Mradi wa Bonde la Ziwa Victoria (LVEMP II) wamefanya ziara katika miradi mbali mbali inayo fadhiliwa na mradi huo katika jiji la Mwanza
Kamati hiyo imepata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo maabara ya kisasa ya maji iliyojengwa katika eneo la igogo katika kata ya Igogo Jijini Mwanza,ambapo kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na mkandarasi.Kamati pia imeridhishwa na kiwango cha malighafi na zana za ujenzi zinazotumika katika ujenzi wa eneo
Katika hatua nyingine kamati ilitembelea mradi wa kuzalisha samaki unaofanyika katika chuo cha uvuvi nyegezi katika kata ya Nyegezi,ambapo kamati ilijionea namna mradi huo unavyoendelea kujengwa,pia kuona mabwawa yaliyojengwa kwa ajili ya kuzalishia vifaranga wa samaki,ambapo zaidi ya vifaranga 30,000 watazalishwa kwa wiki,kwa kutumia teknolojia ya kisasa,mradi utazalisha samaki aina ya sato na kambale.
Pia kamati ilitembelea mradi wa uboreshaji wa machinjio katika eneo la kata ya Mhandu ambapo walishuhudia hatua iliyofikiwa na mkandarasi katika ukarabati huo,pia walipata maelezo ya kina kutoka kwa wahandisi wa Halmashauri ya jiji wanaosimamia mradi huo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.